Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, July 16, 2025

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.

                          .....Kikosi cha Damu chafu
Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakala kushoto akimkabidhi mfanowa hundi ya Milion 4 Nahodha wa Damu Chafu Saddy Mapuya
                           .......Mapuya akiwa na kombe



 Rais Ayub akiwa na vijawa wake wakizunguka uwanja wa Saba saba wakati timu yake ikisaka ushindi

.......Rais Ayub wa mbele aiyechutama akiwaongoza vijana wake kuomba dua siku moja kabla ya fainali kwenye maskani ya timu hiyo
......Rais Ayub akiwashukuru mashabiki baada ya timu yake kuibuka mabingwa

                                       Rasis Ayubu akizungumza na Mtandao huu juzi

       

       Na Dustan Shekidele. Morogoro.

MTANDAO Mpendwa wa shekidele umeandaa makala Maalum ya Michuano ya Planet Ndondo Cup iliyotamatika hivi karibuni Mkoani hapa,kwa timu ya Damu Chafu kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa huo  mara mbili mfurulizo.

 

Awari ya yote pongezi za kipekee ziwafikie waandaji wa michuano hiyo kituo cha Planet Redio chenye Makao yake Makuu Ghorofa la Mt Uluguru lililopo Mtaa wa Mlapakolo Kata ya Mji Mkuu .

 

Redio hiyo inayomilikiwa na Fred Mlingo ambaye baba yake  mzazi ndiye Mlikiki wa Ghorofa hilo la hotel ya kisasa ya Mt Uluguru takribani miaka 4 mfurulizo ametoa kibali kwa vijana wake kuandaa mashindao hayo chini ya Nahodha wao Mkurugenzi wa vipindi Madam Warda Makongwa.

 

Ligi ya Msimu huu ilishirikisha timu 4 ambazo ni Wakushi Fc Kutoka kata ya Mafiga.Chaka Bovu Fc kutoka Kata ya Kiwanja cha Ndege,Black People’Taifa la Watu weusi’ kutoka Kata ya Mji Mpya na Mabigwa watetezi Damu Chafu Fc Kutoka kata ya Mwembesongo.

 

Timu hizo ziliingia moja kwa moja  Nusu fainali ambapo Dmu Chafu walitinga fainali baada ya kuinyuka kwa mikwaju wa Penalti Black People huku Chaka Bovu  walitinga fainali kwa njia hiyo hiyo ya Mikwaju ya Pelnati dhidi ya Wakushi Fc baada ya timu zote hizo kutoka sare  dakika 90 za awari.

 

Kwenye mchezo wa Fainali uliohudhurika na mashabiki kibao waklongozwa na mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe Mussa Kilakala,Chaka Bovu walijaa kwenye mfumo wa Damu Chafu na kujikuta wakipokea kichapo cha bao 3-0 hali iliyopelekea kichaka chao kibovu kilichonyauka njasi kuunguzwa na Damu hiyo chafu.

 

Mara baada ya kutetea ubingwa huo walioutwaa Mwaka jana Damu Chafu walikabidhiwa zawadi wa Kombe na kitita cha Pesa Milioni 4 na Mgeni rasmi Mhe Kilakala.

 

Kufuatia timu hiyo kuweka rekodi ya mashindano hayo kutwaa kombe hilo mara mbili mfurulizo Mtandao huu ulitinga kwenye maskani ya Damu Chafu Mtaa wa Mafisa Kata ya Mwembesongo kwa lengo la kujua siri ya mafanikio ya timu hiyo kwenye mshindano hayo.

 

Baada ya kufika  kwenye maskani ya timu hiyo iliyopo jirani na geti kuu la shule ya Msingi Mafisa A Mtandao huu ulirakiwa na Rais wa timu hiyo Ayub Aziz

 

Rais huyo alipotakiwa kueleza siri ya mafanikio hayo alisema  ni umoja wa wachezaji, Viongozi na wananchi wa kata ya Mwembesongo,ambapo makundi yoye hayo yaliungana kwa hali na mali na kufanikisha jambo hilo.

 

“Siri kubwa ya sisi kutwaa kombe hili mara mbili mfurulizi ni kama ifuatavyo wachezaji na viongozi wa timu zote zilizopo kata ya Mwembesongo tumeweka kando tofauti zetu tumeungana kwa kushirikiana na wananchi wa kata hii kufanikisha jambo hilo.

 

Timu zilizopokata ya Mwembesongo ni Burnafaso Fc. Mangolo Fc. Assemble fc na Chadongo Fc”amesema Rais huyo na kuongeza.

“Kitu kingene ambacho wengi hawakijui namua kukuambia wewe shekidele ni kwamba ukuta mzima wa  Damu Chafu  wanalala na kuamka hapa Mafisa.

 

Mabeki hao ni Saddy Mapuya ambaye ni Nahondha .Said Mwande,Hamza Beta na Abuutwaribu Chachallo huyu ni kiungo mwingine ni mshambuliaji Jafaph Kipira”alisema Rais Ayub

 

Amesema wachezaji hao 5 ambao wapo kikosi cha kwanza mbali ya kuwa wachezaji kwa umuhimu wao wanaingia kwenye vikao vya  viongozi ndio maana wanachezaji kwa kujitoa zaidi wakiwa na mapenzi ya dhati na timu yao ya Mtaani.

 

Alipoulizwa pesa hizo Milioni 4 wamezifanyia nini? Rais Ayub alijibu

 

”Kwa sababu swala hili lilikuwa la Kata tukisaidiwa na wananchi hivyo tumeamua kurejesha sehemu ya pesa hizo kwa kulipa Luku na bili za Maji kwenye misikiti 5 ya Kata ya Mwembesongo, kisha tumesoma dua ya kuwarehemu marehemu dua hiyo imekwenda sambamba na sadaka ya chakula, pesa zilizobaki tumewapa posho wachezaji na kulipa madeni”alimalizia kusema Raia huyo wa heshima.           

                    


 

 

 

 

Tuesday, July 15, 2025

KIJIWE NONGWA. UKIONA KAFUTA BANGO UJUMBE UMEFIKA












 

 

Na Mpekunyuzi wa Mitandao Dunstan Shekidele.

Kama kawaida mtumishi wako, kila wiki naweka Bando linalonitembeza kwenye Mitandao ya Kijamii kukusanya jumbe mbali mbali.

Miongoni mwa jumbe hizo ni za Kuelimisha, Kukosoa na Maneno ya hekima yanayotukumbusha kuwa jirani na Mwenyezi MUNGU.

Tukutane Wiki Ijayo kwa mabango Mengine yenye Jumbe Moto Moto.

Friday, July 11, 2025

UTUNZAJI MAZINGIRA NISHATI SAFI CUP KUPANDA MITI 14500 MOROGORO

    Mwandishi wa Mtandao akiwa juu ya Mlima Uluguru Mgeta Wilaya ya Mvomero
Mwandishi wa Mtandao huu akiwa juu ya Milima hiyo ya Uluguru akiangalia shamba a matunda ya kizungu ya Kauberi. Mwandishi huyo alipanda juu ya Milima hiyo lliopo Manispaa ya Morogoro na Usafiri wake wa Pikipiki.

.....Mwezi ukichomoja  Milima ya Uluguru Majira ya saa 12 na nusu Jioni
......Mpiga picha wa Mtandao huu alipiga picha hii akiwa chini ya Milima ya Uluguru Mtaa wa Area Five Nane nane Manispaa ya Morogoro

Mkurugenzi wa Shirika hilo  Gration Mbelwa [kushoto] akiwa na Katibu  Mkuu wa Chama Cha Boda boda Mkoa wa Morogoro  Francis  Kayombo [Kati mwenye frana nyeupe  ni Mjumbe wa Bodi ya shirika hilo Hussein Ngurungu ambaye ni mchezaji wa zamani wa Pan Afrika na Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars.

Ifahamike Mzee Ngurungu ameitumikia timu hiyo ya Taifa kwa miaka 12 mfurulizo  rekodi hiyo aliyoiweka miaka ya 80 mpaka 90 haijavunjwa na mchezaji yoyote mpaka sasa.

 

 



                                Kamati ya Mashindano hayo

          

           Na Dustan Shekidele,Mogogoro.

KATIKA hali ya kurejesha ubora wa Milima ya Uuguru ambayo ni chanzo kikuu cha maji yanayosambaa  Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es salaam.zaidi ya miche  14500 ya Miti inatarajiwa kupandwa juu ya Milima hiyo ikiwa ni jitihada za serikali kuleta mabadiriko juu ya matumizi  ya Nishati safi na utunzaji wa Mazingira.

 

Shughuri hiyo iliyoandaliwa na Shirika isilo la kiserikali la Mother Of  Mercy linakwenda sambamba na michuano ya Mpira wa Miguu itakayoshirikisha timu 32 kutoka Kata zote 29 za Manispaa ya Morogoro.

 

Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw Gration Mbelwa amesema  mbali na Mashindano hayo yaliyopewa jina la  Nishati safi Cup pia kutakuwa na mshindano ya Boda boda.

Akifafanua zaidi mbele ya Waandishi wa habari Mbelwa amesema.

 

 “kila timu itakayoshiriki  mashindano hayo itapanda miche  500 nia ni kurudisha hali ya hewa kuwa salama huku lengo ni uhamasishaji wa wananchi juu ya matumizi ya Nishati safi” amesema Mkurugenzi huyo na kuongeza kudadavua jambo hilo.

 

“Licha ya michuano ya Mpira wa miguu  kutakuwa na mashindano ya bodaboda ambapo mshindi wa kwanza tutamkabidhi bodaboda mpya huku mshindi wa pili akinyakua kitita cha milioni 1 na mshindi wa tatu ataondoka na laki 5,na kila mshiriki wa bodaboda atapanda mti mmoja kwenye Milima hiyo”alimalizima kusema Mkurugenzi huyo.

Ifahamike miaka ya 70 Milima hiyo ya Uluguru ilikuwa na Mandhari nzuri huku ikitiririsha Maji sehemu mbali mbali za Milima hiyo.

 

Kufuatia hari hiyo Mwanamuziki Maarufu barani Afrika Mwenyeji wa Morogoro Hayati Mbaraka Mwinshehe aitunga wimbo wa kusifu Manzari nzuri wa Milima hiyo.

 

Kuanzia Miaka ya 2000 Milima hiyo ilianza kupoteza uzuri wake kufuatia baaadhi ya wenyeji wanaoishi juu ya Milima hiyo kuchoma Moto kwa kile kichotajwa kuandaa mashamba yao wanayolima juu ya Milima hiyo kando kando ya Mito hiyo inayotiririsha maji kuelekea Mikoa hiyo ya Pwani, Dar es salaam na Morogoro.

 

Baada ya kushamili kwa Vitendo hivyo vya uchomaji Moto aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Morogoro Miaka hiyo Mhe Dkt Nibuka Mzeru kwenye moja ya Michango yake Bungeni aliiomba serikali kuwahamisha wananchi wanaoishi juu ya Milima hiyo.

Kauli hiyo Mzeru ambaye ni Mluguru Og ilipigwa Vikari na waluguru wanaoishi juu ya Milima hiyo.wakiitaka serikali kama itakubari ushauri huo basi zoezi hilo la kuhamisha wananchi wanaoishi juu ya Milima lifanyike nchi nzima.

Baadhi ya wananchi wa wamelipongeza shirika hilo kwa kupanda kiwango hicho kikubwa cha miti kwenye Milima hiyo.

“ Binafsi nalipongeza sana shirika hilo kwa jambo hilo zuri wanalokwenda kulifanya ushauri wangu kwao wahakikishe miti hiyo inakuwa hivyo wanaopoipanda imwagiliwe maji ili isife kama unavyojua mvua vimekata jua ni kali”amesema Juma Athumani

                      

 


KAZI INAENDELE KWA KASI MKANDARASI KAMUA KULING’O LILE DARAJA LILILOKATIKA,

              Daraja  la zamani baada ya kukatika hali ilikuwa hivi
Madent wa Shule ya Msingi Kaloleleni wakigombea kuvuka kwenye daraja hilo la muda



           Muonekana wa sasa baada ya daraja la awari kuondewa

         

           Na Dustan Shekidele.Mogoro

ILI kupata uwanja mpana wa kufanya kasi kwa haraka, wakandarasi wa Kampuni ya COPE iliyopewa jukumu la kujenga daraja kubwa a Relwe Maarufu daraja la Ng’ombe ameamua kuliondoa daraja la zamani na kutengeneza daraja la muda upande wa kulia wa Mto Morogoro.

 

Ikumbukwe mwezi ulipita daraja hilo lilikatika na kukata mawasiliano ya watumiaji wa daraja hilo wananchi wa kata za Mji Mpya na o Kichangani.

 

Hali hiyo ilisababisha usumbufu kwa watu mball ikiwemo wanafunzi wa shule za Sekondari na Msingi pamoja na wazee wasiojiweza wanaotunzwa na serikali kwenye  kambi ya Funga funga.

 

Juzi Mtandao huu  ulitinga kwenye daraja hilo kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo na kuwahabarisha wananchi  hususani wananchi wa kata za Mji Mpya na Kichangani wanautumia daraja hilo ambalo ni kiunganishi muhimu cha kata hizo mbili ambazo ni Maarufu Mkoani  Morogoro.

 

Baada ya kufika Mtaa wa Makaburi ‘A’ kata ya Mji Mpya lilipo daraja hilo Mtandao huu ulishuhudia watu mbali mbali wakiwemo wanafunzi wa shule ya Msingi Kaloleni wakigombea kuvuka kwenye daraja  la Muda kama wanavyoonekana pichani.

Wahenga wanasema ‘kujisifu sio dhambi  dhambi ni kuziendekeza hizo sifa’.

 

Mara baada ya daraja hilo kukatika Mtandao ndio ulikuwa wa kwanza kuripotia habari hiyo.sasa hapa siziendekezi hizo sifa ndio maana naendele kuwapa mwendelezo wa ujenzzi wa daraja hilo mara kwa Mara.

 

Mtandao huu utafanya hivyo mpaka daraja hilo litakapokamiika.

 

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...